Saturday, February 18

Ikwiriri - Tanzania

    Kuna wiki moja na ushee tulikua kimya kidogo, lakini kimya hicho kiliambatana na kusafiri kwetu kwenda kutembelea sehemu mbalimbali. Moja ya sehemu tulitembelea ni Ikwiriri, iliyopo mkoa wa Pwani.
   Moja ya sifa za sehemui hii ni upatikanaji wa nazi. Nazi twajua zina matummizi mbalimbali kwa binadamu na moja wapo ni kutengeneza mafuta ya kupaka mwilini ambayo haswa hutumiwa na watoto wachanga, watoto wadogo na hata watwazima.              
                                                                                                       
                                               
                               

  Matumizi mengine ni hutumika kama kiungo katika mapishi ya mboga na hata ya wali. Kuna wanaotumia tui la nazi kupikia chapati... ushawahi kuzila? kuzitengeneza je? tutakuja kukufahamisha zaidi kuhusu mapishi haya.
   Nazi hutumika pia katika kutengenezea chetna, yaani ni chachandu ya machicha ya nazi , na hili pia tutaja wajuza namna ya kutengeneza.





Iwapo umesafiri na kuweza kupata historia, matukio mbalimbali tunakukaribisha kushare nasi kupitia menutimes@gmail.com 

Kutoka Ikwiriri enu Time inaarifu

No comments:

Post a Comment