Wednesday, October 12

Mapichi ya Sandwich

Kuna Rafiqs zangu ambao hawapendi kusimama muda mrefu jikoni ili kuandaa mlo, na kuna wengine ambao wanahitaji kujua menyu ipi wanaweza kutengeneza, kula na kushiba lakini watumie muda mchache katika utengenezaji huo.
Nimeona niwajuza namna ya kutengeneza Sandwich, ambayo itakugharimu takribani dakika 20 tu.

Mahitaji:
  • Kitunguu maji - 1
  • Pilipili hoho - nusu
  • Nyanya iliyosagwa - 1
  • Maziwa  - robo kikombe
  • Butter kiasi
  • Olive oil - vijiko 3
  • Mayai - 4
  • Cheese (jibini) iliyosagwa/ ya maji kiasi
  • Weka kikaangio jikoni, kisha washa moto, ongeza mafuta acha yachemke, weka vitunguu maji na chumvi kiasi
  • Ongeza pilipili hoho, huku unakoroga
  • Andaa mayai kwa kuyakoroga kwenye kibakuli pembeni, ongeza na chumvi kidogo sana, kisha changanya kwenye kikaango kilichopo jikoni, koroga kwa kuyavuruga vuruga
  • Baada  ya hapo ongeza maziwa na jibini katika mchanganyiko wote, endelea kukoroga vyema mpaka mayai yanapoanza kuiva
  • Ongeza nyanya iliyosagwa (au nyanya ya kopo), koroga vyema mchanganyiko wako mpaka mayai yameiva vyema
  • Epua mayai yako kwani yako tayari
  • Chukua vipande vyako vinne vya mikate, uvioke kidogo kwenye toster
  • Paaka butter upande mmoja ya mkate (waweza tumia peanut butter pia)
  • Weka vipande vya matango kwenye upande mmoja wa mkate
  • Weka mchanganyiko wa mayai yaliyoiva vyema
  • Ongezea na kipande kimoja cha smoked beef
  • Malizia kwa kuweka kipande cha pili cha mkate juu yake
  • Kata sandwich yako tayari kwa kuliwa
Chagua kinywaji chochote cha kushushia, iwe maji safi, Coca-cola, maziwa, wine n.k yaani ni wewe tu na chaguo lako. Waweza kula sandwich muda wowote iwe asubuhi, mchana, usiku au kama snack yaani chakula cha kupitisha muda. Pia waweza kumtengenezea mwanao kama lunch yake pale akiwa shule.
unaionaje??? tuma maoni yako kupitia menutimes@gmail.com

No comments:

Post a Comment