Thursday, September 29

Kitaani zaidi - Kilimanjaro

Nkaona nikiwa Kilimanjaro, hapa Moshi kwanini nisijaribu kuonja kuku wa kienyeji ambao wamechomwa, nikahabarishwa kuna chaka moja wanafahamika vyema kwa shughuli hii.
Tulipofika mie na mwenyeji wangu kwanza tulikuta kuna kuku wazima wamewekwa kwenye jiko, tulipoagiza nusu, ndo mpishi akaongeza ndimu na chumvi na viungo vingine kisha amkaushe vyema tayari kwa kuliwa. Mpaka hapo nkapata hamu ya kujua zaidi mapishi yake, ila kutokana na wingi wa kazi tulishindwa fanya mawasiliano.
Mwisho wa shughuli sahani huonekana namna hii

Pembeni wanaweka matango, nkaamini mboga mboga muhimu kwenye chakula. karibuni Moshi.

No comments:

Post a Comment