Monday, July 11

Mapishi ya leo

Bado nipo safarini, nimetua Mwanza nasubiri kuelekea Bukoba. Wakati huu nasubiri, nataka kushare nanyi menyu niliyopika siku ya Jumamosi.
Kuku asiye na mifupa  na viazi mviringo vya kuponda a.k.a boneless chicken and mashed potatoes.

Mahitaji:
  • Kuku asiye na mifupa 1 mzima
  • Vitunguu swaumu vilivyosagwa
  • Pilipili manga
  • Chumvi kiasi
  • Vinegar
  • Olive oil
  • Viazi mviringo
  • Kitunguu maji 1
  • Blueband
  • Maziwa kikombe kimoja
  • Butter kiasi
Changanya vitunguu swaumu, chumvi kiasi, oilve oil kiasi, pilipili manga kiasi, vinegar kiasi, na ndimu. Kisha katakata kuku wako katika vipande vya wastani. Changanya kuku na mchanganyiko huo hapo juu. Waweke kuku waliochanganywa kwenye jokofu a.k.a fridge kwa muda wa dk 30 ili ule mchanganyiko uweze ingia kwenye nyama ya kuku kwa uzuri zaidi.

Baada ya dakika hizo toa kuku, waweke kwenye kikaangio cha kwenye oven kama kwenye picha:
    Pika kuku wako katika nyuzi joto 190, na kwa muda wa dakika 30 - 40.Baada ya dakika kama 20 wageuze ili pande zote ziweze iva vyema.
    Epua kuku wako, waache wapoe kwa dk 10, kisha watayarishe tayari kwa kuliwa.
    Kupika viazi ya kuponda,
    Hatua: Menya viazi vyako, kisha vioshe na kuviweka jikoni. Ongeza maji safi, na katakata kitunguu maji na uweke ndani ya viazi. Ongeza chumvi kidogo na pilipili manga kidogo kupata ladha flani tamu. Hakikisha kuvigeuza ili viweze kuiva kwa urahisi. Vikishaiva, epua sufuria na mwaga maji, kisha chukua mwiko na kuanza kuviponda. Ongeza maziwa, siagi a.k.a blueband na butter kisha endelea kuviponda. Endelea kuongeza maziwa, siagi na butter mpaka utakapoona viazi vimelainika vya kutosha. Tayarisha mash potatoes yako kwa kuliwa
    
    Tayarisha menyu yako kwa kuliwa, yangu ilifanana hivi:
    Karibuni kutufundisha kupika menyu mbalimbali. Naamini Bukoba tutajifunza kupika ndizi.........

2 comments:

  1. mdau,nimeipenda hii menu nataka ipika naomba nielekeze jinsi ya kuto mifupa hao kuku au je kuna sehem wanauzwa wakiwa wameshatolewa mifupa?kama ndio plz elekeza mimi

    ReplyDelete
  2. Hawa kuku wasio na mifupa wanapatikana kwenye supermarkets mathalani Shoprite. Ila waweza kumtoa minofu wewe mwenyewe pale kabla hujampika. Ukishamwosha unakata minofu ukitenganisha na mifupa, na kisha unaipika ile nyama ikiwa haina mifupa. Naamini nimekujibu vyema.

    ReplyDelete