Upishi wake ni rahisi sana, karibu tujifunze:
Mahitaji:
- Mnofu wa samaki usio na mfupa
- Chumvi kiasi
- Unga wa ngano kiasi
- Mayai mawili
- Chengachenga za mikate a.k.a bread crumbs
- Mafuta safi ya kupikia.
Hatua:
- Tayarisha unga wa ngano kwenye sahani ya pekee yake, changanya na chumvi kidogo, (na iwapo utapenda ladha ingine kama viungo vya pilau n.k. basi changanyia humo)
- Koroga mayai na yaweke kwenye sahani ya peke yake
- Weka chenga chenga za mikate kwenye sahani ya pekee
Muonekano utakua kama hivi hapo chini:
Unga wa ngano wenye chumvi (na viungo kama utapenda)
Mayai yaliyokorogwa
Chenga chenga za mikate a.k.a bread crumbs. Waweza zinunua madukani au ukaanga mikate kisha kuikwaruza kupata chengachenga
Mnofu wa samaki usio na mfupa tayari kwa kupikwa
- Mkate samaki wako vipande viwili ili aweze kuenea vyema kwenye kikaangio chako, kisha chukua kipande kimoja weka kwenye sahani ya unga wa ngano, ukihakikisha pande zote zimelowekwa na unga wa ngano. Kung'uta kipande cha samaki kuhakikisha unga uliobakia vibaya umetoka wote.
- Weka kipande cha samaki kilicho na unga wa ngano kwenye mayai yaliyokorogwa ukihakikisha pande zote zimepata kulowekwa na mayai, kung'uta mayai yanayodandia kipande
- Malizia kukiweka kipande ndani ya sahani yenye chengachenga za mikate huku ukihakikisha pande zote zimelowekwa na chengachenga hizo. Kung'uta kuondosha mabakio ya chengachenga zilizodandia
- Weka kipande cha samaki katika chombo kisafi, kisha fanya hivyo hivyo kwa vipande vilivyobakia
- Viache vipande hivyo kwa muda kama wa nusu saa kabla ya kuvipika
Muonekano wa vipande vya samaki baada ya hatua hizo utaonekana kama hapo chini
- Weka kikaangio jikoni, hakikisha kimepata moto, kisha ongeza mafuta ya kupikia kiasi na yaache yapate moto pia
- Weka kipande cha samaki kwenye kikaango na ukiache kwa muda wa dakika tatu hivi kwa kila upande kipate kuiva vyema
- Samaki wako atakua tayari kwa kuliwa
Muonekano wa samaki akiyekaangwa utaonekana kama hivi hapo chini
Kwenye mbogamboga, nilikua na karoti, njegere, maharagwe machanga, brokoli, ambapo vilichemshwa pamoja kidogo kisha kuchanganywa na salad dressing na kuwekwa kwenye jokofu vipate ubaridi.
Muonekano ni kama huo hapo chini
Kwenye chipsi, kama kawaida tunachemsha viazi kwa mda mfupi sana vikiwa na chumvi na kitunguu maji kisha twavikaanga kwenye mafuta moto.
Ushuhuda wetu ni kama hapo chini kwa picha
Na mwisho...... sahani ya baba ilionekana hivi, ikisindikizwa na maji ya matunda ya maembe, tomato sauce pamoja na mayonnaise.
Tujuze umeyaonaje haya mapishi na utakapo yajaribu mapishi haya share nasi muonekano wake utakavyokuwa, na kama wanafamilia au marafiq ambao utakao waandalia wameonaje mapishi haya.
Tunawatakia kila la kheri Alhamisi hii, ambayo ni mwanzo wa wikiendi.
No comments:
Post a Comment