Monday, June 13

Dar es Salaam

Shawarma zapatikana Dar Es salaam sehemu mbalimbali. Zamani kidogo ilinipasa kusubiri mpaka maonesho ya sabasaba ndo niweze kupata kula Shawarma, lakini siku hizi, Victoria, mikocheni, City center na sehemu kadhaa zinapatikana.

Shawarma ni sandwich ya kiarabu ambapo chapati au mkate ya duara laini  hutumiwa kuvingirishwa nyama   (aidha ya mbuzi, kondoo, kuku, ng'ombe au mchanganyiko wa vyote) ndani yake pamoja na vionjo vingine 
Nyama hii huwekwa kwenye jiko maalumu na kuokwa taratibu kwa muda mrefu. Nyama ya nje inapoiva hukwanguliwa na kuacha ya ndani ipate nafasi ya kuiva.
Moja ya sehemu walinionesha kidogo namna wanavyotengeneza........ Karibu!!

  • Hapa Shawarma ipo jikoni inaendelea kuiva taratibu.....,



  •  Na baada ya  dakika 30 Shawarma ikawa imeiva vyema tayari kwa kuliwa.


  • Chapati spesho zinatayarishwa kwa kupashwa moto, maana tayari zinakuwa zilishapikwa:

  • Vipande vya nyama vilivyookwa na kuiva vyema vinawekwa ndani ya chapati iliyofunguliwa:



  • Mchanganyiko mwingine unaongezwa hapa, ambao sikuweza upata wote:


  • Shawarma imefungwa na kuviringishwa ndani ya karatasi laini linalisaidia isidondoke na iwe rahisi kubeba. Kwa yule ambaye angependa kula pale pale ipo tayari kwa kuliwa:


  • Kwa atakaye penda kuibeba a.k.a Take away basi wanaifunga vyema namna hiyo:


3 comments:

  1. pande za sweden wanaiita tutila inaongezwa vitunguuu nyanya na vimahindi vya kuchemsha tamu saana

    ReplyDelete
  2. kwa dar inapatikana wapi mdau? umeandika tu mikocheni,victoria na city center but where exactly.....plzzz

    ReplyDelete
  3. Nisamehe kwa kuchelewa kukujibu ila inapatikana mkabala na kituo cha mafuta kilichopo Victori. Upande wa pili kuna apartments na restaurant flani kwa chini. Fika hapo rafiq na utapata shawarma.

    ReplyDelete