Tuesday, May 24

Usiku wa leo - Rosti ya Maini & Chapati

Tena nimeingia jikoni kuweka mkono wangu katika mapishi ya usiku wa leo. Niliamua kupika Rosti ya Maini na Chapati. Kwa kujua nimelipikaje rosti hilo tafadhali angalia Mapishi time. Chapati ni kwa hisani ya Bakhresa, zapatikana kwenye Supermarkets nyingi tu mjini hapa, hivyo nilifanya kuzikaanga tu.
Karibuni...
 

2 comments:

  1. sasa unatufundisha kupika chapati kwa kuchukua za bakhresa,kwanini usionyeshe ufundi wako kwa kuipika toka mwanzo ?jipange upya my dear!weka mapishi uliyofannya mwenyewe sio ya dukani!

    ReplyDelete
  2. Kwanza kabisa tukushukuru kwa kuchukua muda wako na kuangalia blog yetu. Asante sana!! Pili ikumbukwe kwamba mbali na kufundisha namna ya kupika, timu ya Menutime pia wana kazi ya kutangaza bidhaa za watanzania kwani twajivunia utanzania wetu. Hivyo basi tungeweza kuonesha namna ya kupika chapati toka mwanzao (na tutaonesha siku za usoni,) ila kwa hapa nia ni kuelezea pia kuwa hizi hatukuzipika sisi, bali tumenunua toka kwa Bhakresa. Hatuoneshi ufundi wetu bali tunafundisha wenzetu wasiokua na ujuzi namna mbalimbali ya kupika vyakula mbali mbali, na sio kujionesha!
    Tumeonesha migahawa mbalimbali wapi Rafiqs wanaweza pata menyu zao, tunaonesha pia bidhaa zitokanazo sokoni, supermarket na kadhalika. Hatujifungi upande mmoja wa kuonesha namna ya kupika tu laah, tuelewe vyema tulishajipanga tulipofikiria kuanzisha blog,hivyo basi tuliamua na tunaweka mapishi ya popote tunapokutana nayo.
    Asante kwa maoni, na pia inaonesha una ujuzi zaidi juu ya mapishi mbalimbali, karibu share nasi ili nasi tuwajuze wengine. Email address yetu ni menutimes@gmail.com. karibu sana our dear!

    ReplyDelete