Monday, August 29

Salad yenye jibini

Bado naendele na matumizi ya jibini a.k.a cheese, na leo naongelea utengenezaji wa salad yenye jibini. Kuhusu wingi na uchache wa uwekaji wa jibini hii itategema na mapenzi yako. Kuna wengine hawapendi sana ni vyema kutumia kidogo, na wengine wapenda muno, hivyo nakushauri uweke inayokutosha wewe.

Mahitaji:
  • Vitunguu maji 2
  • Nyanya 3
  • Letuce 1
  • Karoti kubwa 1
  • Limau 1
  • Chumvi kidogo
  • Vinegar nyeupe
  • jibini iliyokwaruzwa
Hatua:
  • Katakata vitunguu maji, kisha vioshe na maji yenye chumvi kupunguza harufu
  • Katakata nyanya, letuce kisha changanya na vitunguu maji
  • Kwaruza karoti katika ukubwa uupendao, kisha changanya na mchanganyiko wa hapo juu
  • Kamua limau na changanya juisi yake na mchnganyiko huo hpo juu, kisha ongeza chumvi kidogo
  • Weka vinegar nyeupe kidogo kunogesha salad yako
  • Malizia kwa kuweka jibini uliyokwaruza katika wingi uupendao
  • Changanya mchanganyiko huo hadi uone vyote vimechanganyika vyema.
Weka ndani ya jokofu kwa mda vipate kupoa vyema tayari kwa kuliwa. Waweza kula salad yako na chi[s, mihogo, pilau au mlo mwingine uupendao wewe.
Kwa wale wanaofanya zoezi la kula kidogo ili wasiongezeke mwili, wanaweza kula vivyo hivyo ila wawe makini na uwekaji wa jibini.

No comments:

Post a Comment